Saturday, July 30, 2011

Man U mtalipa kisasi au mta........


 Mabingwa wa Champions League yaani Barcelona, wanayo shuguli nzito kwa kipindi mwisho wa mwezi wa saba na mwezi August barani America.
 Wakiwa bara la Amerika watakutana na timu tatu tofauti moja kati ya timu hizo ni mashetani wekundu yaani Man Utd.
 Ingawa Sir. Alex, kocha wa timu ya Man U bado hajaonyesha imani yake nakikosi chake lakini DeGae amesikika akijitapa na kuisifia timu yake kuwa anaamini itatoka na ushindi mkubwa kwenye mechi hiyo itakayo chezwa tarehe 31 mwezi huu.
 Wadau wa mpira wa miguu duniani akiwemo Pele, wanaufananisha mchezo huu kama vita vya malipizi maana ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 28 mwezi Mei mwaka huu timu hizi zilikutana kwenye fainali za kombe la Champions League.
 Matokeo ya fainali ile yaliiacha dunia nzima ya mpira wa miguu midomo wazi baada ya Man U kupokea kichapo cha magoli 3-0, mmoja kati ya wakali walioiumiza Man U wengine hupenda kumuita DOKTA yaani Messi hatokuwepo kwenye kikosi cha Barca baada ya kuwa yupo kwenye likizo kwao Argentina.
 Barca watakuwa wakicheza 4-3-3, akiwemo Valles, Abidal, Pique, Puyol, Fontas, Thiago, Benquet, Iniesta, Afellay, Jonathan bila kumsahau Villa.
 Pia Man U itasukuma mtanange huu ikiwa inacheza 4-3-3, ikimchezesha De Gae, Vidic, Ferdinand, Evra, Young, Carrick,  Anderson, Park,Berbatov, Rooney.
 Barcelona pia wakiwa bado bara la Amerika watachuana na CD Gadalajara mnamo tarehe 3 August na Club America mnamo tarehe 6 August.
 Usiku wa kuamkia leo nahisi jiji letu litakuwa na shamsham sana, yaani tukimaliza tu shngwe za fiesta 2011, usiku mzito tutakuwa tanapagawa na mechi hii kati ya Man U na Barca pale Washington DC.
                                                                                                      Masekepa Asangama