Monday, August 1, 2011

Nicki Minaj anmwiga Lil`mama kweli....????


 Ni juzi juzi tu mwanadada mkali wa hip pop duniani yaani Lil'mama alitanabaisha kuwa yeye ni Trendsetter, yaani kiongozi wa style ya nywele anayoitumia sana mwana hip pop mwenzake Nicki Minaj.
 Zaidi lil mama alisema kuwa Nicki Minaj alianza kutumia mtindo huo wa nywele mara tu baada ya kuhudhuria moja kati ya maonyesho ya lil mama lililoitwa Amarican best dance crew.
 Lil mama kwa msisitizo alisema sio tu mtindo huo wa nywele anaotumia Nicki Minaj, bali ni vitu vingi watu wanaiga kutoka kwake, mfano alisema style yake ya ukali kwenye kurap ambayo pia Nicki amekuwa akiitumia sana, pia aliongeza kwa kusema kuwa hata jinsi anavyovaa na jinsi anavyoandaa mziki wake watu huiga sana toka kwake.
 Ila rapper huyo ameeleza furaha yake kuona watu wengi wakiiga mambo yake na kueleza kuwa hiyo inaonyesha kuwa yeye ni mzuri sana ndo mana watu wengi wamekuwa wakimuiga.
                                                                                                            Masekepa Asangama.