Monday, August 1, 2011

Jay Z na Kanye kwenye album moja.......

 Nakubali kuwa mwanahip-pop Jay-Z anahusishwa na hili swala la mpinga kristo yaani Freemaso lakini bado siwezi kumhesabu nje ya waasisi wa mziki wa hip-pop na anayewika mpaka leo hii.
 Bado anazikamata hisia za mashabiki wengi duniani kwa kila nyimbo anayoachia kwenye industry hii ya muziki.
 Hivi karibuni akiwa na rapper ambaye na yeye anahusishwa na mambo ya Freemason hapa namzungumzia Kanye west, wametangaza tarehe rasmi watakayoingiza sokoni album yao mpya walioifanya pamoja.
 Marafiki hawa kwenye moja ya mahojiano walisema album hiyo iitwayo "The throne" itaingia sokoni tarehe 8 August, wamesema kuwa itaanza kuingia iTUNES na siku nne baadae yaani tarehe 12 August wasambazi wengine wataipoata pia album hiyo.
 Wamesisitiza mashabiki wao kuwa ndani ya album hiyo kutakuwa na mazuri zaidi ya wanchokisikia kwenye moja ya nyimbo ambayo wameshaitoa iitwayo "Otis" wakimshrikisha mkali wa RnB Otis Redding.
 Hivyo basi kwa wale mashabiki wa wanahip-pop hawa yani Jay na Kanye, tukae mkao wa kula mnamo tarehe nane ambayo kwa hapa TZ itakuwa sikukuu ya nananane tuingie iTunes na tununue album hiyo iliyosubiriwa kwa muda mrefu.
                                                                    Ian.

Amber asema na wanaopenda kupiga picha za.......!


 Kwenye dunia ya leo ni swala la kawaida rafiki, ndugu jamaa na zaidi zaid wapenzi kupigana picha ambazo kwa ukawaida zinakuwa kama hali ya kufurahia maisha yao au kwa ajili ya kumbukumbu muhimu.
 Hii huwa rahisi zaidi kutokana na uaminifu uliopo kati yako na mwenzako, sio hivyo tu hata kushare simu, laptops na mara nyingine unaweza kukuta watu ambao wako kwenye mahusiano wanapeana passwords za simu, emails na hata password za ATM ili panapotokea ulazima inakuwa rahisi kujikimu kifedha.
 Lakini mwanamitindo maarufu na mpenzi wa zamani wa rapa Kanye west swala la uaminifu kwa rafiki na watu wake wa karibu halikuzaa matunda na badala yake kuleta matatizo kwenye maisha yake mara baada ya watu aliyowaamini sana kusamabaza picha zake za siri kwenye mitandao bila idhini yake rasmi.
 Kwa kinywa chake mwanamitindo huyo alisema maneno makali na yenye mafunzo ndani yake ambayo ni salama kama rafiki utayapata pia.
 Amber alisema;
"I trusted someone who worked for me and allowed them to use my lap top millions times, i cought them sending my pics to themselves. I fired them immediately. Wiz and i and both our families knows have know abowt this for a month now.
 These pics are 2 and half years old, when i just sit in my computer am realy hurt, i have too many young girls who are looking up to me. I wouldnt have put these pics my self.
 The company that i was working with no longer wants me to work with them because of these pics and prevents me to get money to take care of my family. It is messed up situation when someone comes into ur life and and tries to destroy it.
 I know i am not the only girl in the world that has taken pics like that but they were very private.
 I am very sorry for letting my young rosebuds down, please understand that was result of trusting a person that didnt deserve my trust. I have cried for the past two two days but i know this too shall past, thank u all for ur support"
 Kuna mwenye swali, hope hakuna ila kama upo tuma kwenda email ya Bloglab enterprices, na utapata majibu.
                                         John Masunga Didas.

Nicki Minaj anmwiga Lil`mama kweli....????


 Ni juzi juzi tu mwanadada mkali wa hip pop duniani yaani Lil'mama alitanabaisha kuwa yeye ni Trendsetter, yaani kiongozi wa style ya nywele anayoitumia sana mwana hip pop mwenzake Nicki Minaj.
 Zaidi lil mama alisema kuwa Nicki Minaj alianza kutumia mtindo huo wa nywele mara tu baada ya kuhudhuria moja kati ya maonyesho ya lil mama lililoitwa Amarican best dance crew.
 Lil mama kwa msisitizo alisema sio tu mtindo huo wa nywele anaotumia Nicki Minaj, bali ni vitu vingi watu wanaiga kutoka kwake, mfano alisema style yake ya ukali kwenye kurap ambayo pia Nicki amekuwa akiitumia sana, pia aliongeza kwa kusema kuwa hata jinsi anavyovaa na jinsi anavyoandaa mziki wake watu huiga sana toka kwake.
 Ila rapper huyo ameeleza furaha yake kuona watu wengi wakiiga mambo yake na kueleza kuwa hiyo inaonyesha kuwa yeye ni mzuri sana ndo mana watu wengi wamekuwa wakimuiga.
                                                                                                            Masekepa Asangama.