Friday, July 29, 2011

Nicki Minaj na Roman Zolanski ni TWINS!!!!



 Licha ya umaarufu alionao Nicki Minaj, vituko na habari tofauti kumuhusu zinazaliwa kila kukicha.
 Hivi karibuni ametoa kali baada ya kumtambulisha dada yake ambaye ni pacha wake, Nicki Minaj akiwa kwenye moja ya mahojiano kwenye kituo maarufu cha matangazo kijulikanacho kama VIBE, alinukuliwa akisema "the one you see in buttoms up song with Trey, thats not Nicki Minaj, instead she is Roman Zolanski".
 Ina maana muda wote ulimwengu ukidhani kuwa yule ni Minaj, yeye mwenyewe alikana na kusema yule si yeye ni pacha wake Roman Zolanski.
 Pia alitanabaisha kuwa mama yao anasikika kwenye remix ya nyimbo ya romans revenge akirap sehemu ndogo kwa lafudhi ya kiingereza cha ya uingereza.
 Zaidi Minaj alisema "Roman was born inside me, i become her when i get ungry, she is a demon inside me".... Pia wanaharakati wa hip pop wamemfananisha Roman na Slim shady ambaye nayeye ni demon wa Eminems.
 Ndio sababu remix ya nyimbo ya Romans revenge, mwanadada Minaj aliamua kuwakutanisha wakali hawa yaani Roman Zolanski na Slim shady.
 Swala ni kwamba je kwa hapa TZ wapo wasanii wanaowajua ndugu zao kwa maana ya mizuka yao, na kuwatumia vizuri.... Au ni bangi tu mwanzo mwisho?
                                                                                           Baadae rafiki zangu,
                                                                                                                    Ian.