Friday, July 29, 2011

Tusiharibu mimba, watoto ni faraja kubwa.....

 Jina langu ni "baba wawili", ni kijana wa kawaida kabisa na ili kuthibitisha ukawaida wangu jamani hata kazi maalum sina, ila hilo sio tatizo sana kwangu.
 Ishu ni hawa madogo wawili "mapacha" wangu, ambao niliwapata nikiwa mdogo sana.... Na hiyo ndio sababu leo timu ya bloglab imetoa nafasi hii kwangu ili niwe naandika kuhusu maisha yangu na watoto wangu ili kijana yeyote atakaye soma simulizi hizi apate nguvu kimaisha kuhusu familia na hatma yake namba ya vijana wanaotoa mimba kila siku na hata wanaopoteza maisha kupungua kabisa.
 Kama nlivyokwisha kusema kuwa niliwapata hawa mapacha nikiwa mdogo sana, na mara nyingi vijana kama mimi ambao wanakuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi mara tu linapotokea swala la mimba mahusiano hulegalega sana.
 Sawa hata mimi siwezi kukataa hata mara moja kuwa siku ile mama wawili aliponiambia kuwa anahisi ana ujauzito sikupata mshtuko, HAPANA! Nilipata mshtuko tena mkubwa sana, nakumbuka tulikuwa nyumbani kwangu, hata hamu ya kuendelea kupumzika iliisha na niliamua kuondoka zangu na kumwacha mpenzi wangu chumbani peke yake.
 Sawa sababu ni nyingi sana ambazo humpelekea kijana kupatwa mshtuko na hatma yake kuamua maamuzi hasi ili kuondokana na jambo hilo kabisa, wengine hukimbia mpaka miji ili kuepuka tatizo, wengine hukataa kabisa kuwa hawahusiki na ujauzito huo na wengine huthubutu kufanya "abortion" yaani kuitoa mimba.
 Ila nisingependa kuwa mwalimu kwa kiasi kikubwa bali kusimulia tu maisha yangu na wanangu hawa, ndani ya simulizi hizi pia kijana utapata mambo meengi mazuri na hii itakujenga hata siku utakapo kuwa na hali kama yangu iwe rahisi kuendanna na hali hiyo.
 Doto anaitwa "Dido" na kulwa "Obama", nawapenda sana..... Mara nyingine natamani wawe marafiki zangu na kuutoa huu ubaba kabisa labda wangenipenda zaidi na kuniamini bila kuwapo chembe ya uoga kuwa mi ni baba ntawachapa au ntawakasirikia...
 Naamini sio rahisi ila sitochoka kuwajengea imani hiyo ndo maana hata ukija nyumbani siku moja utasikia wananiita "kaka", na naamini ipo siku wataniita rafiki pia.
 Wameleta faraja kubwa kwenye familia yangu, faraja ambayo mimi na mama yao hatukuwa nayo kabla... Sasa ndani ni furaha tu, Dido atacheza hivi Obama vile basi ni furaha tupu jamani....
 Nakaaga na kuwaza je mimi na mama yake tungeamua kuitoa mimba, watoto hawa wangekuwa wapi leo.... Je! Furaha hii tungeipata wapi tena, hakika tusingeipata popote. Basi kumbe ulikuwa uamuzi wa busara sana kutokuikana mimba.
 Ingawa ulikuwa uamuzi mzito sana, kwani sikuwa na kazi, mama pia hakuwa na kazi.... Wapi tungepata pesa za kuwalisha watoto hawa? Kila jibu lililokuja wakati hule lilikuwa tatizo. Lakini tulipiga moyo konde na kuamua kuilea.
 Haya leo ngoja niishie hapa.... Ila jamani vijana wenzangu "mimba" msizitupe...... Mtoto huwa neema kubwa jamani, natamani mngeniona na furaha yangu leo.
                                                                                                         Tukutane wiki ijayo
                                                                                                                   Baba Wawili