Saturday, July 30, 2011

Luda ana zaidi ya show na swagg "TUJIFUNZE"


 Mshkaji anaitwa Christopher Brian Bridges kwa jina kamili, nimejiuliza hii aka ya Ludcriss ilikujaje nakosa jibu sahii, maana haifanani kabisa na jina lake halisi....
 Jamaa alizaliwa mwaka 1977, Sep 11 pale Champaign nchini U.S.A...
 Alianza mziki 1998 na leo ana album saba na leo atakuwa na bonge moja la concert hapa jijini kwenye viwanja vya Leaders Club.
 Najua marafiki wengi tutakuwa pale usiku huu, ila kama rafiki nimewaokotea kastory nataka kushare na nyinyi kumhusu Luda.
 Kama nlivyokwisha sema kuwa hii ni album ya saba ya msanii huyu, inaitwa "Battle of sexes" ambayo aliiachia tarehe 9, march mwaka huu.
 Idea ya album hii ilikuwa kuwakutanisha Luda na mmoja kati ya wasanii walio chini ya lebo yake iitwayo "disturbing the peace au DTP". Yani kama unavyoona Lil'wayne alivyokuwa na Nicki Minaj kwenye album yao mpya.
 Mapema kabla ya kumaliza kurekodi album hiyo ambayo kabla yakupewa jina la battle of sexes ilipewa jina la back to back, mwanadada huyo kwa jina la Shawnna alivunja mkataba na lebo ya Luda na kuhamia kwenye lebo ya T-Pain iitwayo Nappy boy Ent.
 Kuhama kwa mwanadada huyo kulivuruga sana ratiba za Ludacriss na kupelekea kuanza upya kurekodi album hiyo na kuiita Batte of sexes.
 Licha ya tatizo hilo Luda alifanikiwa kumaliza kurekodi album hiyo na tarehe 8 Dec 2009 alichia ngoma ya kwanza kutoka kwenye album hiyo na nyimbo hiyo "how low" ilifanya vizuri na mwanzo wa mwaka huu aliachia album na ilifika mauzo ya Gold baada ya kuuza nakala 137000 kwa wiki ya kwanza sokoni.
 Swala linakuja Je! Ingekuwa ni msanii wa bongo falva kakutwa na matatizo kama hayo angemaliza kurekodi hiyo album kweli?
 Hakika HAPANA, zaidi wangeishia kulumabana kwenye vituo vya habari na kutupiana maneno tu mwisho kuharibu heshima zao na vipaji vyao pia,
                                                                                                            Africa Nyumbani.