Saturday, July 23, 2011

Jamani Gucci Mane sio mmiliki wa kampuni ya GUCCI....


 Saba kati ya wajanja kumi wa mtaa wanaamini kuwa Gucci Mane msanii wa hip pop nchini marekani ndiye mmiliki wa GUCCI kampuni ya mavazi kama ilivyo kwa Sean Combs aka P.Diddy na kampuni yake ya SEAN JOHNS.
 Siajabu hata wewe piw ni mmoja kati ya hao wanaoamini hivyo ila ukweli ni kwamba Gucci mane na GUCCI ni mambo mawili tofauti kabisa.
 Ili kukuweka sawa kuhusu hili leo ntakupa ukweli kuhusu GUCCI, kwanza kabisa mmiliki wa kwanza au mwa nzilishi wa kampuni ya GUCCI ni Guccio Gucci mzawa wa Florence Italy.
 Kabla ya kuanzisha kampuni hiyo Guccio alikuwa mfanyakazi katika baadhi ya mahoteli makubwa sana mjini Paris na London pia, akiwa huko bwana Guccio alipenda sana uzuri wa mabegi yalikuwa yanaingia na wageni toka nchi mbalimbali.
 Aliporudi kwao Italy  akaamua kufungua duka dogo amblo waliuza viyu kama mabegi, viatu, wallets, set cover za magari n.k. Hapo ndipo mwanzo wa kampuni ya GUCCI.
 Baadae akishirikiana na wanawe watatu wakiume yaani Aldo, Vasco na Rodolfo waliweza kufungua maduka zaidi kwenye miji mashuhuri duniani  mfano Milan, Rome na baadae New York Marekani.
 Ingawa pametoke kampuni nyingi za mavazi duniani bado GUCCI imekuwa juu sana, na mpaka sasa ina zaidi ya maduka 237 dunia nzima.
 So kwa habari hiyo kwa ufupi naamini tumefunguka sana kuhusu hivi vitu.