Saturday, July 23, 2011

Aibu, saa saa simusimu jaman...

 Siku moja nilikuwa kwenye daladala, natoka zangu chuoni naelekea hostel. Ndani ya lili gari kuna mmoja kati ya masuperstar wetu wa bongo jina naomba nilihifadhi.
 Nikamuuliza “samahani kaka, sasa  hivi ni saa ngapi?”. Jibu alilonipa mmmhh nikamvua vyeo vyote jamani….. uanjua alinijibu nini!!!!!
 Eti “ooh sorry, simu yangu haina charge dadangu, siunajua mambo ya mgao wa umeme” hahahahahahha, jamani siku njema na hao mastar wenu…..
                                                                                                                  Sara Sean

Jamani Gucci Mane sio mmiliki wa kampuni ya GUCCI....


 Saba kati ya wajanja kumi wa mtaa wanaamini kuwa Gucci Mane msanii wa hip pop nchini marekani ndiye mmiliki wa GUCCI kampuni ya mavazi kama ilivyo kwa Sean Combs aka P.Diddy na kampuni yake ya SEAN JOHNS.
 Siajabu hata wewe piw ni mmoja kati ya hao wanaoamini hivyo ila ukweli ni kwamba Gucci mane na GUCCI ni mambo mawili tofauti kabisa.
 Ili kukuweka sawa kuhusu hili leo ntakupa ukweli kuhusu GUCCI, kwanza kabisa mmiliki wa kwanza au mwa nzilishi wa kampuni ya GUCCI ni Guccio Gucci mzawa wa Florence Italy.
 Kabla ya kuanzisha kampuni hiyo Guccio alikuwa mfanyakazi katika baadhi ya mahoteli makubwa sana mjini Paris na London pia, akiwa huko bwana Guccio alipenda sana uzuri wa mabegi yalikuwa yanaingia na wageni toka nchi mbalimbali.
 Aliporudi kwao Italy  akaamua kufungua duka dogo amblo waliuza viyu kama mabegi, viatu, wallets, set cover za magari n.k. Hapo ndipo mwanzo wa kampuni ya GUCCI.
 Baadae akishirikiana na wanawe watatu wakiume yaani Aldo, Vasco na Rodolfo waliweza kufungua maduka zaidi kwenye miji mashuhuri duniani  mfano Milan, Rome na baadae New York Marekani.
 Ingawa pametoke kampuni nyingi za mavazi duniani bado GUCCI imekuwa juu sana, na mpaka sasa ina zaidi ya maduka 237 dunia nzima.
 So kwa habari hiyo kwa ufupi naamini tumefunguka sana kuhusu hivi vitu.
 Wengi wetu kiukweli licha ya kuwa mashbiki wa msanii lil`wayne hatujui ukweli kumhsu baba yake mzazi. Hali hii imekuwa hivi kutokana na baadhi ya rafiki kudhani kuwa baba mzazi wa lil`wayne ni Bird Man.
 Ukweli ni kwamba baba mzazi wa star huyu wa hip pop ni Dwayne Michael Carter, ambaye alifariki wakati lil`wayne alipokuwa mdogo sana.
 Lil Wayne pia alipewa jina hilohilo la Dwayne, lakini kwasababu hakupata kabisa malezi ya baba aliamua kuitoa D na kubakisha wayne tu… na mpaka leo anatumia jina hilo.
 Kali zaidi kuhusu wayne ni kwamba alipata motto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 15…… duh hii ni balaaa, kumbe mpaka ulaya watoto huzaa watoto.
                                                                                                         Nice times rafiki