Monday, August 1, 2011

Jay Z na Kanye kwenye album moja.......

 Nakubali kuwa mwanahip-pop Jay-Z anahusishwa na hili swala la mpinga kristo yaani Freemaso lakini bado siwezi kumhesabu nje ya waasisi wa mziki wa hip-pop na anayewika mpaka leo hii.
 Bado anazikamata hisia za mashabiki wengi duniani kwa kila nyimbo anayoachia kwenye industry hii ya muziki.
 Hivi karibuni akiwa na rapper ambaye na yeye anahusishwa na mambo ya Freemason hapa namzungumzia Kanye west, wametangaza tarehe rasmi watakayoingiza sokoni album yao mpya walioifanya pamoja.
 Marafiki hawa kwenye moja ya mahojiano walisema album hiyo iitwayo "The throne" itaingia sokoni tarehe 8 August, wamesema kuwa itaanza kuingia iTUNES na siku nne baadae yaani tarehe 12 August wasambazi wengine wataipoata pia album hiyo.
 Wamesisitiza mashabiki wao kuwa ndani ya album hiyo kutakuwa na mazuri zaidi ya wanchokisikia kwenye moja ya nyimbo ambayo wameshaitoa iitwayo "Otis" wakimshrikisha mkali wa RnB Otis Redding.
 Hivyo basi kwa wale mashabiki wa wanahip-pop hawa yani Jay na Kanye, tukae mkao wa kula mnamo tarehe nane ambayo kwa hapa TZ itakuwa sikukuu ya nananane tuingie iTunes na tununue album hiyo iliyosubiriwa kwa muda mrefu.
                                                                    Ian.